Ufugaji wa nondo wa hariri nchini Iran

Kiswahili Radio 118 views
Mkoa wa Gilan kaskazini mwa Iran ni kati ya mikoa iliyo mstari wa mbele katika ufugaji wa nondo wa hariri.

Ufugaji wa nondo wa hariri hatimaye hupelekea kupatikana uzi wenye thamani kubwa wa hariri.

Ufugaji huo umeweza kufanikiwa mkoani Gilan kutokana na hali nzuri ya  hewa katika eneo hilo.

Ufugaji wa nondo wa hariri unahitaji kiwango kidogo tu cha mtaji na ardhi. 

Hariri na bidhaa zipatikanazo kutokana na hariri kutumika katika sekta mbali mbali za viwanda kama vile viwanda vya petrokemikali na vipodozi.

Iran ni nchi ya tano kwa ufugaji hariri duniani baada ya China, India, Uzbekistan, Thailand, Brazil, Vietnam na Korea Kaskazini.

Add Comments