Serikali ya Libya yashambulia ngome za wanamgambo wa Haftar

Kiswahili Radio 8 views
Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya inayoongozwa na Fayez al-Sarraj imefanya mashambulio makubwa dhidi ya ngome za wanamgambo wanaoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar kusini mwa mji mkuu Tripoli.

 Libya ina serikali mbili hasimu, moja ikiwa na makao yake mjini Tobruk, iliyoko karibu na Jenerali Haftar, na nyingine ya Serikali ya Mapatano ya Kitaifa Libya inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Libya ilitumbukia katika machafuko na vita vya ndani baada ya wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na wale wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kuishambulia nchi hiyo na kusaidia harakati za kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi Muammar Gaddafi hapo mwaka 2011.

Add Comments