Siku ya Kimataifa ya Quds

Kiswahili Radio 7 views
Miaka 41 iliyopita, Imam Khomeini, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds.

Moja ya matunda ya muqawama huo wa wananchi Waislamu uliokuja baada ya Imam Khomeini kutangaza Siku ya Kimataifa ya Quds, ni kukimbia wanajeshi wa Israel katika ardhi za kusini mwa Lebanon pigo ambalo lilikuwa baya sana katika historia ya Israel kwani kwanza ilivunja ile ngano potofu kwamba Wazayuni hawashindiki na pili nyoyo za wananchi wa ulimwengu wa Kiarabu zilifufuka na kuanzia wakati huo ulimwengu wa Kiarabu ulianza kupata uhai mpya. 

Add Comments